Wednesday, November 3, 2010

Dr. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar...


Amani imetawala Zanzibar wakati Dr. Ali Mohammed Shein, akiapishwa ramsi leo kuwa Rais wa saba wa Zanzibar. Hafla hizi zimefanyika katika viwanja vya Amani Zanzibar zikiongozwa na mgombea urais wa bara kwa tiketi ya CCM Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wananchi wa Zanzibar wamepewa mapumziko katika siku hii maalumu ili kushuhudia halfa za kumuapisha Dr. Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Tuesday, November 2, 2010

John Mnyika kiulaini...


Mgombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA atangazwa rasmi kuwa mbunge tawala wa jimbo la Ubungo baada ya kumshinda mgombea mwenza Hawa Ngumbi kwa zaidi ya kura 66,700.

VURUGU ZA UCHAGUZI MWANZA ZALETA HASARA KWA RAIA WEMA

Pichani ni Bwana Jimmy Luhende mmiliki wa gari lililochomwa mwoto katika vurugu za uchaguzi mkoani Mwanza










Gari la Bwana Jimmy Luhende aina ya Land Cruiser lilichomwa moto katika eneo la ofisi za halmashauri ya jiji la Mwanza wakati Bw. Luhende akiwa ndani ya jengo hilo akifanya kazi ya uangalizi na ufuatiliaji wa uchaguzi na kuhesabu kura. Bwana Jimmy Luhende ni mwanaharakati wa masuala ya sera.

HOFU YA MATOKEO KUCHAKACHULIWA, WANANCHI MWANZA WACHOMA MOTO OFISI ZA CCM - NERA



Mara baada ya matokeo ya vituo kuwekwa hadharani, wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, walianza kupita mitaani kwa kushangilia. Lakini muda si mrefu walianza kufanya fujo za kuchoma matairi na hatimae kufikia kuchoma ofisi za CCM eneo la Nera mkoani Mwanza baada ya kusubiri sana kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi. Sababu kubwa ilielezwa kuwa wananchi hawa walikuwa na wasiwasi kuwa matokeo yangechakachuliwa. Lakini ukweli halisi kutoka eneo la kuhesabu kura zinasema kuwa, kuhesabu kura kulichukuwa muda kwani kila karatasi ilikuwa inapitishwa kwenye mashine ya kuscan ili kuondoa wasiwasi wa kugushi ama kuchakachua matokeo. Wananchi walipaswa kuelezwa haya yote kuepusha vurugu zisizo kuwa za msingi.

Monday, November 1, 2010

MATOKEO YA AWALI YANAPOTANGAZWA






Jijini Mwanza, baadhi ya wafuasi wa chama cha upinzani cha DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), mara baada ya matokeo ya awali kutangazwa.