Tuesday, March 23, 2010


MKUU WA MKOA WA MARA MHE. ENOS MFURU AKISALIMIANA NA MKURUGENZI WA UTPC KATIKA WARSHA YA WADAU NA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA ILIYO FANYIKA MKOANI MARA MAPEMA MWEZI WA TATU. MHE. MFURU ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA WARSHA HIYO

BAADHI YA WAFANYAKAZI KUTOKA UTPC WAKIWEKA TAJI KATIKA MOJA YA MAKABURI YA WALIO UWAWA KWA KUPIGWA NA MAPANGA MKOANI MARA.

BAADHI YA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI KILIMANJARO (MECKI) WAKIWA KATIKA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA OFISI YAO KUFUNGULIWA TENA BAADA YA KUFUNGWA KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA MIGOGORO NDANI YA KLABU HIYO. KLABU HIYO ILIPATA UFUMBUZI WA MGOGORO WAO MAPEMA MWEZI WA PILI MWAKA HUU BAADA YA KAMATI YA MUDA KUUNDWA AMBAPO KAMATI HIYO ITAFANYA KAZI MPAKA KUFIKIA NOVEMBA MWAKA HUU UCHAGUZI MKUU UTAKAPO FANYIKA

MKURUGENZI WA UTPC BWANA ABUBAKAR KARSAN AKIJIBU HOJA KATIKA WARSHA YA WADAU NA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI ILIYO FANYIKA MJINI MOSHI MAPEMA MWEZI WA PILI TAREHE 19. WARSHA HII ILILENGA KUTOA NAFASI KWA WADAU NA WAANDISHI WA HABARI KUJADILIANA KUHUSU MAHUSIANO YAO KWA AZMA YA KUTATUA MATATIZO YANAYO WAKABILI KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI.

WAVUVI KATIKA WILAYA YA UKEREWE, WAKITAFUTA KITOWEO KWA AJILI YA FAMILIA NA BIASHARA. WANATAMBUA KUWA KUNA 'KILIMO KWANZA' LAKINI MAZINGIRA WANAYO ISHI WAMEZUNGUKWA NA MAJI HIVYO UVUVI KWAO NI FIRST PRIORITY

NILIPIGA PICHA HII ASUBUHI NILIPO AMKA KWENDA KUPIGA MSWAKI. MLIMA HUU UNAVUTIA HAKIKA UNASTAHILI KUPEWA JINA "THE ROOF OF AFRICA"