WAPO WANAO KERWA NA BAADHI YA MAMBO YANAYOTOKEA NCHINI KWETU NA WANATOA
MITAZAMO YAO KAMA INAVYO ONEKANA HAPO CHINI.
MTAZAMO HUU UMETUMWA NA BWANA JIMMY LUHENDE
Nimetizama mjadala wa leo katika Star TV kwa makini kaka Mabuga Paul.
Maoni yangu kwa haraka haraka:
Serikali ya JK inajitafuna yenyewe, je, unajua kuwa JK alikuta mfumuko
wa bei wa 4.5 ? yeye ameufikisha zaidi ya 10 ? Sasa ni wachumi wa
serikali yake, BOT na waziri husika wanaotakiwa kuulizwa! Kimsingi
Rais, Waziri na BOT ndio wamewasaliti wafanyakazi. jamani, joto hilo
si kwa wafanyakazi tu bali kwa kila mtanzania.
Unawezaje kushughulikia mishahara ? mishahara ni matokeo ya kazi,
mapato na mfumuko wa bei. ukiwa na uozo katika hayo, watu watapata
mishahara ambayo haiwezi kukidhi mahitaji yao muhimu. Ukiwa na wachapa
kazi, mapato mazuri na ukayakusanya vizuri na ukaziba mianya ya
udokozi na ukaeza kudhibiti wa mfumuko wa bei, Basi utaweza kulipa
mishahara ya watu wako na wakaweza kupata huduma muhimu.
Watu na Viongozi makini hawajadili mishahara kabla ya kujadili pato la
serikali,kodi na mifumo yetu ya kukusanya na kudhibiti kodi. Kuna
mahali tumechemka ! Kuna wasomi wa Uchumi wanaliosema kuwa Ukiongeza
mishahara utaongeza mfumuko wa bei. Nadhani hii ni Keynesian theory,
nakumbuka kitu kama hiki katika somo la uchumi nililosoma kidato cha
sita miaka kama kumi iliyopita.
Watumishi wa umma wa TZ wako sawa kabisa kudai mishahara kwani hilo
ndio tatizo lao kwa sasa na ambalo wanataka lishugulikiwe (immediate
problem). Pia lipo katika Uwanja wao! Ni kazi ya wengine kuwaelimisha
na wakati huo ni kazi ya wengine Kushughulikia hayo mengine. Au
tuwaongezee mishahara kwanza kisha tufanye jitihada za kushughulikia
hayo mengine pamoja na elimu ya umma. Pia Tunatakiwa kukubali kuwa
Tumechemsha pahala fulani na Wahusika wakiri kwa dhati.
Ninashangaa CCM hawajaliona kama agenda katika kikao chao cha jana
kwani bendera yao ina jembe, kwa maana ya kumuwakilisha mfanyakazi.
Ninashangaa pia mtu kusema "ni kikundi kidogo kinataka kufanya siasa."
Ni kweli kuwa ni kikundi kimoja kidodo kwani huwezi kutegemea wafanya
kazi wote (zaidi ya 300,000) wakutane na rais au waje studio, kwanza
wakija wote ni maandamano tosha. Wanaonesha kuwa wamekomaa kwa kutuma
na kuuamini uongozi wao. Hayati Nyerere hakuenda kudai uhuru na
watanzania wote, walienda wachache kwa niaba ya wengi. Mbona wabunge
wamefunga mijadala Bungeni bila kutuuliza? Ni kwa sababu tumewapa
mamlaka hayo! Hatuhitaji kuenda wote pale (watu milioni 40). Itakuwa
na maana kuwa hatuna imani na wabunge wetu. Kuhusu siasa, kila kitu ni
siasa! siasa ndipo inaweka miundo na watu wa kufanya utendaji katika
miundo hiyo. Kila penye watu zaidi ya mmoja kuna siasa ya aina yake.
Kanisa na na Misikiti ina siasa, hata nyumbani kuna siasa wakati
tunafanya maamuzi. Na huwezi kuzungumzia sera, viongozi, uongozi,
utawala na vipaumbele katika nchi na useme kuwa huzungumzii SIASA,
suala la Mishahara ya watumishi ni SIASA katika ngazi ya Taifa na
halitaki majibu mepesi.
Ninashangaa zaidi kusikia mkuu wa nchi akisema kutaneni nashauri ataje
saa siku na muda na awaamuru kama mkuu wakutane na kisha wamuambie
yale waliyoshindwa kufikia muafaka au wampatie mapendekezo ili yeye
afanye maamuzi mazito.
watu makini jadilini!
Jimmy
Friday, April 9, 2010
Thursday, April 8, 2010
DAMPO JUMLISHA MAKAZI YA WATU JUMLISHA WANYAMA
PICHANI NI DAMPO LILILOKO MKOANI TANGA MAENEO YA DUGA AMBAPO LINATAKA KUBORESHWA KUWA DAMPO LA KIMATAIFA (SAFI SANA). LAKINI CHAKUSHANGAZA DAMPO HILI LIPO KARIBU NA MAKAZI YA WATU NA VILEVILE MALISHO YA WA WANYAMA KAMA INAVYO ONEKANA PICHANI, CHA AJABU KULIKO VYOTE, WAPO WATU WANATUMIA MADIMBWI YALIYOKO KATIKA ENEO HILI LA DAMPO KWA KUOGA NA KUFUA. AJABU WATANZANIA TUNAELEKEA WAPI... MAGONJWA YA MILIPUKO YATAISHAJE KWA STYLE HII
MADAWA YA KULEVYA - TANGA
HIZI SIO CHOKAAAAA AU VIFURUSHI VYA CHUMVI. NI SEHEMU YA SHEHENA YA KILO 95 ZA HERON ZILIZOKAMATWA MKOANI TANGA TAREHE 08/03/2010 ZIKISAFIRISHWA KWENDA DAR ES SALAAM. HAPA MAAFISA WA KIKOSI KAZI CHA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA WAKIPAKIA DAWA HIZO KATIKA MABOX TAYARI KUZIPELEKA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI ZAIDI WA KITAALAMU
Wednesday, April 7, 2010
KAZI ZA ASKARI POLISI NI NYINGI
BANGI TARIME
Subscribe to:
Posts (Atom)