Sunday, September 19, 2010

RIZIKI YA Bi ZAINAB MOHAMED KATIKA DAMPO LA NSAGALA UYOLE, MBEYA



Pia katika Dampo hili Nsagala-Uyole Mbeya, nilikutana na Bi, Zainab Mohamed mjane mwenye umri wa miaka 45 na watoto wanne. Mama huyu anakusanya chupa katika mifuko midogo midogo na kuuza mfuko mmoja kwa shilingi 300.
Bi, Zainab alipo ulizwa ni mtaji kiasi gani anahitaji ili aweze kufanya biashara ambayo si hatarishi kwa afya yake, Bi, Zainab alisema kuwa shilling 50,000 itamtosha kufungua biashara ambayo haitakuwa hatarishi kwake.
Mama huyu anaingia katika dampo hili kila siku kuanzia saa 12 asubuhi na kutoka saa moja jioni.

1 comment:

  1. Strength of a woman.

    Inasemekana kazi si kuzaa bali ni kulea.Ndio huyu mama kaamua kufanya biashara hii ili kumuuezesha kulea wanawe.It is so sad.
    Si hata wanao uziwa hizo chupa waweza wasaidi watu kama hawa kwa kuwanunulia nguo maalumu za hii kazi.
    Like gumboots,gloves,apron/overall,mask na vinginevyo vitakavyo mmzuiia mtu asiumie katika kazi.

    Ama basi kwa makampuni yanayonunua chupa hizo iwaajiri watu kama hao...wanaweza fungua ofisi mahali watupaji taka wanaweza leta chupa nao wapeleke kwa mashini zao.

    Mola atupe njia

    Nogrecia Nangena (Encubed)
    Nairobi - Kenya

    ReplyDelete