Monday, November 16, 2009

Wakufunzi, Wahariri wa habari msiache kuandika

Na Victor Maleko

Wahariri wa vyombo vya habari na Wakufunzi wanaofundisha kwenye tasnia ya habari nchini wamehimizwa kuwa mfano wa kuigwa kutoa elimu ya habari kwa njia ya kuandika habari, fursa itakayowafanya waoneshe umahiri wao kwa wanafunzi wanaowafundisha.

Changamoto hiyo ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga kwenye mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili ya Wakufunzi wa tasnia ya habari, yaliyofanyika Jijini Mwanza hivi karibuni.


BAADHI YA WAKUFUNZI WAKIJADILI JAMBO KATIKA MAFUNZO HAYO

Bw. Kajubi ambaye alikuwa mmoja wa wawezeshaji wawili wa mafunzo hayo ya siku mbili alisema, Wahariri na Wakufunzi wa tasnia ya habari hawawezi kuwa na ujasiri wa kuyakosoa mapungufu ya habari zinazoandikwa na waandishi wao kama hawaandiki kila mara.
"Siku hizi, Wahariri wa vyombo vya habari na Walimu wa fani ya uandishi wa habari hamuandiki kabisa! Sasa mnapata wapi ujasiri wa kutambua kisha kuhariri upungufu wa habari zinazoandikwa na Waandishi wengine?!" alishangaa Bw. Mukajanga.

Aliwaambia jumla ya washiriki 11 wa mafunzo hayo kwamba kutoandika habari za kawaida na makala katika magazeti kunahatarisha ukuaji wa tasnia ya habari kwa sababu viongozi wanaotarajiwa kuonesha mfano na umahiri wa kuandika hawatimizi wajibu wao.

Akizungumzia maandalizi ya baadhi ya wanafunzi kuwa Wahariri, Bw. Mukajanga ambaye ni Mwandishi mzoefu aliyewahi kumiliki gazeti, alitahadharisha kuwa, “Msijidanganye kwa kudhani kuwa mtu yeyote anaweza kujiita Mhariri pasipo kuwa na ujuzi wala uzoefu wa uandishi wa habari za kawaida na makala" .

Naye Mwezeshaji mwenza, Bw. Fili Karashani, alieleza kushangazwa kwake kuwaona baadhi ya wahitimu wa elimu ya juu katika tasnia ya habari hawawezi kuandika habari, jambo ambalo alisema, hulazimika kuwafundisha upya jinsi ya kuandika habari wahusika hao wawapo makazini.

Kwa upande wake, Mhariri wa gazeti la ‘Msanii Afrika’ na Jarida hili, Bw. Calvin Jilala alisema, uhalali wa mtu aliyepewa dhamana ya Uhariri kufanya kazi yake unatokana na uandishi bora wa habari unaomwezesha kukuza upeo wake wa kutambua usahihi, ukweli, uwazi na umakini wa hali ya juu ya mwandishi husika.

“Kimsingi Mhariri na Mkufunzi wa taaluma ya habari ni Mwandishi wa habari, hivyo si sahihi Mhariri ama Mkufunzi kuacha kazi yake kwa sababu tu kapanda daraja. Hiyo ndiyo kazi yake ya msingi. Wakumbuke wao ni viongozi wanaopaswa kuwa mfano wa kuigwa na wanaowaongoza.” Alisema Bw. Jilala.

Mafunzo hayo yaliwashirikisha Wahariri na Wakufunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali vinavyofundisha elimu katika Tasnia ya habari ikiwemo Mawasiliano ya umma, uandishi wa habari na kadhalika.

Wednesday, November 11, 2009

FAMILIA YA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA ALBINO
NI KATIKA KIJIJI CHA NANDA WILAYA YA BUKOMBE MKOANI SHINYANGA AMBAPO MAMA HUYU NI MKE WA BWANA CHARLES MASANGWA KARAMJI. BWANA CHARLES MASANGWA NA NDUGU YAKE WA KUZALIWA BWANA EMMANUEL MASANGWA WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA KUFANYA MAUAJI YA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO). PICHANI NI MKE WA BWANA CHARLES MASANGWA AMBAYE AMEACHIWA WATOTO SABA, HAO NI WANNE KATI YAO.

Tuesday, November 10, 2009

LAIVU BILA CHENGA
STENDI YA MABASI SHINYANGA

HAPO NI ABIRIA AKIGOMBANIWA NA MAKONDAKTA WA MABASI. KUIBIWA NJE NJE!
ABIRIA WAKISUBIRI USAFIRI - MISUNGWI
STAND NDOGO YA MISUNGWI

SIKU ZA WIKI WATOTO WENGI WENYE UMRI HUU WANAKUWA SHULENI WAKISOMA, LAKINI MTOTO HUYU ANAFANYA KAZI YA KURUHUSU MABASI YA ABARIA YANAYOINGIA NA KUTOKA
KATIKA STENDI HII YA MABASI. JE, BAADA YA MIAKA 20 TANZANIA ITAKUWA NA WASOMI WA AINA GANI
MTANZANIA KAZINI





HUENDA HAWA WALIKUWA WANAJUA "KILIMO KWANZA" TANGU AWALI LAKINI LABDA KWA KUFANYA MAUZO ZAIDI
ALMASI (MISASI) MISUNGWI KUMEKUCHA



MAJEMBE, SURURU NA SHOKA HAVITOSHI SASA NI MWENDO WA MAGREDA. NYUMBA YA MTU SI THAMANI TENA, NI MWENDO WA KUSAKA MAHELA TU. NA KILIMO KWANZA JE?