Monday, October 18, 2010

Karibu tena Tanzania NADIA LEHMANN


Wageni wanapo kuja TANZANIA, wanakutana na marafiki wengi kutoka nchi mbalimbali na pengine kutoka nchi moja.
Wageni hawa hupokelewa vizuri na WATANZANIA wakarimu. Watafanya kazi na WATANZANIA na wataishi nao kama ndugu wakijifunza mengi kuhusu TANZANIA, na siku ya kuondoka TANZANIA watajumuika na WATANZANIA kuwashukuru WATANZANIA na hatimaye wanapofika makwao watoe sifa zote nzuri kuhusu TANZANIA...

NA HIVI NDIVYO WATANZANIA TUNAVYOISHI NA WAGENI WETU...

Kiswahili na Waswahili


Kwa sisi tunaotumia usafiri wa daladala, ni wazi kwamba lazima utoe nauli... Ukijifanya umesahau basi unasoma tu hapo "ABILIA TOA ELA" na hicho ndicho KISWAHILI kwa WASWAHILI... Karibu.

Vijana wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakipambana na madereva wanaoegesha magari pasipo stahili


Halmashauri ya jiji la Mwanza inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha madereva wanaegesha magari katika maeneo yanayostahili. Lakini je, hawa vijana wanaofunga cheni magari yaliyo egeshwa vibaya, kwanini wakuache mpaka uegeshe gari vibaya ndipo wakufuate kukufunga cheni ama ni kwanini hakuna vibao maalumu vya kuwaelekeza madereva maegesho maalumu ya magari? TAFAKARI

Wednesday, October 6, 2010

MWAKA MMOJA BAADA YA KUMALIZA DARASA LA SABA



Vijana hawa wanakusanya mchanga maalumu wa kujengea na kuuza. Mchanga huu unakusanywa katika moja ya mifereji inayopitisha maji machafu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza. Eneo hili ni Igoma nyuma ya kiwanda cha Cocacola na karibu kabisa na eneo la mnada wa Ng'ombe. Nilipo wauliza kwanini wako hapa na sio shuleni baada ya kumaliza darasa la Saba? Walinijibu kuwa kuendesha maisha yao wenyewe ni ngumu itakuwaje kuhusu kwenda shule na mahitaji yake... Huyu ndiye mtanzania wa taifa la kesho..