Wednesday, November 3, 2010

Dr. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar...


Amani imetawala Zanzibar wakati Dr. Ali Mohammed Shein, akiapishwa ramsi leo kuwa Rais wa saba wa Zanzibar. Hafla hizi zimefanyika katika viwanja vya Amani Zanzibar zikiongozwa na mgombea urais wa bara kwa tiketi ya CCM Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wananchi wa Zanzibar wamepewa mapumziko katika siku hii maalumu ili kushuhudia halfa za kumuapisha Dr. Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Tuesday, November 2, 2010

John Mnyika kiulaini...


Mgombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA atangazwa rasmi kuwa mbunge tawala wa jimbo la Ubungo baada ya kumshinda mgombea mwenza Hawa Ngumbi kwa zaidi ya kura 66,700.

VURUGU ZA UCHAGUZI MWANZA ZALETA HASARA KWA RAIA WEMA

Pichani ni Bwana Jimmy Luhende mmiliki wa gari lililochomwa mwoto katika vurugu za uchaguzi mkoani Mwanza










Gari la Bwana Jimmy Luhende aina ya Land Cruiser lilichomwa moto katika eneo la ofisi za halmashauri ya jiji la Mwanza wakati Bw. Luhende akiwa ndani ya jengo hilo akifanya kazi ya uangalizi na ufuatiliaji wa uchaguzi na kuhesabu kura. Bwana Jimmy Luhende ni mwanaharakati wa masuala ya sera.

HOFU YA MATOKEO KUCHAKACHULIWA, WANANCHI MWANZA WACHOMA MOTO OFISI ZA CCM - NERA



Mara baada ya matokeo ya vituo kuwekwa hadharani, wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, walianza kupita mitaani kwa kushangilia. Lakini muda si mrefu walianza kufanya fujo za kuchoma matairi na hatimae kufikia kuchoma ofisi za CCM eneo la Nera mkoani Mwanza baada ya kusubiri sana kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi. Sababu kubwa ilielezwa kuwa wananchi hawa walikuwa na wasiwasi kuwa matokeo yangechakachuliwa. Lakini ukweli halisi kutoka eneo la kuhesabu kura zinasema kuwa, kuhesabu kura kulichukuwa muda kwani kila karatasi ilikuwa inapitishwa kwenye mashine ya kuscan ili kuondoa wasiwasi wa kugushi ama kuchakachua matokeo. Wananchi walipaswa kuelezwa haya yote kuepusha vurugu zisizo kuwa za msingi.

Monday, November 1, 2010

MATOKEO YA AWALI YANAPOTANGAZWA






Jijini Mwanza, baadhi ya wafuasi wa chama cha upinzani cha DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA), mara baada ya matokeo ya awali kutangazwa.

Monday, October 18, 2010

Karibu tena Tanzania NADIA LEHMANN


Wageni wanapo kuja TANZANIA, wanakutana na marafiki wengi kutoka nchi mbalimbali na pengine kutoka nchi moja.
Wageni hawa hupokelewa vizuri na WATANZANIA wakarimu. Watafanya kazi na WATANZANIA na wataishi nao kama ndugu wakijifunza mengi kuhusu TANZANIA, na siku ya kuondoka TANZANIA watajumuika na WATANZANIA kuwashukuru WATANZANIA na hatimaye wanapofika makwao watoe sifa zote nzuri kuhusu TANZANIA...

NA HIVI NDIVYO WATANZANIA TUNAVYOISHI NA WAGENI WETU...

Kiswahili na Waswahili


Kwa sisi tunaotumia usafiri wa daladala, ni wazi kwamba lazima utoe nauli... Ukijifanya umesahau basi unasoma tu hapo "ABILIA TOA ELA" na hicho ndicho KISWAHILI kwa WASWAHILI... Karibu.

Vijana wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakipambana na madereva wanaoegesha magari pasipo stahili


Halmashauri ya jiji la Mwanza inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha madereva wanaegesha magari katika maeneo yanayostahili. Lakini je, hawa vijana wanaofunga cheni magari yaliyo egeshwa vibaya, kwanini wakuache mpaka uegeshe gari vibaya ndipo wakufuate kukufunga cheni ama ni kwanini hakuna vibao maalumu vya kuwaelekeza madereva maegesho maalumu ya magari? TAFAKARI

Wednesday, October 6, 2010

MWAKA MMOJA BAADA YA KUMALIZA DARASA LA SABA



Vijana hawa wanakusanya mchanga maalumu wa kujengea na kuuza. Mchanga huu unakusanywa katika moja ya mifereji inayopitisha maji machafu kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza. Eneo hili ni Igoma nyuma ya kiwanda cha Cocacola na karibu kabisa na eneo la mnada wa Ng'ombe. Nilipo wauliza kwanini wako hapa na sio shuleni baada ya kumaliza darasa la Saba? Walinijibu kuwa kuendesha maisha yao wenyewe ni ngumu itakuwaje kuhusu kwenda shule na mahitaji yake... Huyu ndiye mtanzania wa taifa la kesho..

Sunday, September 19, 2010

KASHOGI JUMA NA JUMA SHABANI VIJANA WAWILI WANAOSHINDA JALALANI KUTAFUTA RIZIKI YAO


HAPA NI JALALANI MAHALA AMBAPO VIJANA HAWA WAWILI (KASHOGI JUMA NA JUMA SHABANI) WANAPO LALA MARA BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YAO.


KASHOGI JUMA NA JUMA SHABANI WAKIWA KAZINI JALALANI



Nikiwa mkoani Mbeya niliamua kwenda kutembelea eneo la kuhifadhia taka maarufu kama dampo lilipo eneo la Uyole-Nsalaga mkoani Mbeya.
Nikiwa katika dampo hilo hilo nakutana na vijana wawili Kashogi Juma mwenye umri wa miaka 38 na mwenzie Juma shabani mwenye umri wa miaka 21. Vijana hawa wanaendesha maisha yao kutokana na kile wanachopata kutoka katika dampo hili.
Kashogi na Juma ni wakazi wa Dar es Salaam eneo la Manzese Uzuri na hapa Mbeya katika dampo hili wamekuja kufanya kazi ya kukusanya vyupa chakavu na kuvipasuapasua katika vipande vidogovidogo tayari kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa mauzo. Nilipo wauliza kwa nini kazi hii wasinge ifanya hapo hapo Dar es Salaam ama mikoa ya karibu kama Morogoro? Walinijibu kuwa Dar es Salaam na Morogoro tayari kumevamiwa na vijana kama wao ambao wanafanya kazi kama hii.
Cha kushangaza vijana hawa wanalala hapahapa Dampo kama picha inavyo onyesha. Vijana hawa wako hatarini kupata magonjwa yanayo sababishwa na uchafu kwa kuwa eneo hili lina harufu kali ya vitu vilivyo oza.
Vijana hawa huuza shilingi 80,000 kwa kila tani moja ya vyupa chakavu na shilingi 200,000 kwa kila tani moja ya Vyuma chakavu.
Vifurushi hivi husafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mauzo. Je kuna vijana wangapi wanaweza kuvumilia kufanya kazi kama hii kabla hawajafikiria kuwa wezi na majambazi ili kujipatia kipato. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?

RIZIKI YA Bi ZAINAB MOHAMED KATIKA DAMPO LA NSAGALA UYOLE, MBEYA



Pia katika Dampo hili Nsagala-Uyole Mbeya, nilikutana na Bi, Zainab Mohamed mjane mwenye umri wa miaka 45 na watoto wanne. Mama huyu anakusanya chupa katika mifuko midogo midogo na kuuza mfuko mmoja kwa shilingi 300.
Bi, Zainab alipo ulizwa ni mtaji kiasi gani anahitaji ili aweze kufanya biashara ambayo si hatarishi kwa afya yake, Bi, Zainab alisema kuwa shilling 50,000 itamtosha kufungua biashara ambayo haitakuwa hatarishi kwake.
Mama huyu anaingia katika dampo hili kila siku kuanzia saa 12 asubuhi na kutoka saa moja jioni.

Saturday, September 18, 2010

KIJANA MUSA MARTINI KATIKA DAMPO LA UYOLE-NSAGALA MKOANI MBEYA


Pia katika Dampo hili la Uyole-Nsagala, nilikutana na kijana mwingine anayeitwa Musa Martini, yatima mwenye umri wa miaka 17, Kijana huyu ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Uyole day. Yupo katika dampo hili kutafuta makopo ambayo atayatumia kutengeneza vibatari ambapo kila kimoja huuzwa kwa shilingi 150. Nilipo muuliza kwa nini haendi shule na badala yake yupo kwenye dampo hili kukusanya makopo hayo, alinijibu kuwa shuleni anadaiwa ada ya shilingi 15,000 baada ya kulipa shilingi 5,000 kama ada ya mwaka katika shule hiyo. Ada yake ya mwaka ni shilingi 20,000. Musa Martini hulazimika kukatisha masomo yake kwa baadhi ya siku na kuja katika dampo hili kukusanya makopo na kutengeneza vibatari ili kupata ada ya shule. Musa Martini anaishi na mdogo wake ambaye yeye hakupata bahati kufaulu na kuendelea na masomo.
Fikiri kijana Musa Martini atakusanya makopo mangapi na atengeneze vibatari vingapi atakavyo viuza apate ada ya shule pamoja na hela ya kupata mahitaji mengine ya kibinadamu. Kumbuka kibatari kimoja kinauzwa shilingi 150, na je ni vibatari vingapi vitanunuliwa ili apate kuishi? Huyu ndiye mtanzania wa taifa la kesho.

KIJANA ERICK JACKSON KATIKA DAMPO LA UYOLE-NSAGALA MKOANI MBEYA



Eric Jackson ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 15. Kijana Erick Jackson anaendesha maisha yake ya kila siku kwa kutafuta chuma chakavu katika dampo hili lenye harufu kali na uchafu wa kila aina.
Maisha ya kijana huyu yanaonyesha wazi kua ni magumu kwa binadamu wa kawaida kuishi. Anachokifanya kijana huyu katika dampo hili ni kukusanya vyuma chakavu na baadaye kwenda kuviuza kwa wachuuzi wengine. Erick Jackson anauza vyuma chakavu vyenye uzito wa kilogramu kumi kwa shilingi 1,500.
Inamchukuwa siku nzima kushinda katika dampo hilo ili kupata kilo 10 za vyuma chakavu.
Mtoto Erick Jackson anatumia jembe na mikono yake ambayo haina kinga yeyote kufukua mlundikano wa takataka ili kupata chuma chakavu. Wakati mwingine itamchukua siku mbili mpaka tatu kupata kilo kumi za chuma chakavu. Kwa mantiki hiyo mototo Erick Jackson anatafuta shilingi 500 kwa siku kwa ajili ya kujikimu maisha yake. Je, Mahitaji muhimu ya mwanadamu ambayo ni chakula, malazi na mavazi anayatimiza kwa kiwango gani kama pato lake ni shilingi 500 kwa siku? Maisha ya mtanzania pamoja na kuwa ni umasikini lakini vilevile ni hatari.

Friday, September 3, 2010

UHABA WA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA, CHANZO CHA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KATIKA MWALO WA KAYENZE - MAGU MWANZA




Huu ni mwalo ulioko KAYENZE, MAGU mkoani Mwanza. Mwalo huu unatumika kwa shughuli nyingi kama inavyoonekana katika picha hizi. Wakazi hawa wangepata huduma ya maji safi na salama huu Mwalo ungebaki salama na pengine magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu, kichocho, na mengineyo yangepungua ama kuisha kabisa.

USIKAE HAPA


Je tuamini kuwa aliyevunja maagizo haya hakuelewa lugha ya Kiswahili ama ni tabia tu ya walio wengi kupuuza maagizo...

Thursday, September 2, 2010

UFADHILI KUTOKA MOIL




Ni faraja iliyoje kwa chama cha mpira wa kikapu mkoani Mwanza MRBA kupata ufadhili wa Trak Suit 30 kutoka kwa kampuni ya ununuzi na usambazaji wa mafuta MOIL iliyo jijini Mwanza. Wadau hawa wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mchezo wa mpira wa kikapu unakuwa kwa kutoa misaada mbalimbali. Hivi karibuni timu ya mpira wa kikapu mkoani Mwanza ilisafirishwa na kampuni hii ya MOIL kuelekea Bulyanhulu kwa ajili ya mechi ya kirafiki.

TUZO ZA WAANDISHI WALIOFANYA VIZURI KATIKA UANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA ZIWA VICTORIA.


Lake Victoria Environment Management Project (LVEMP) hivi karibuni waliandaa mashindano ya muandishi bora wa habari za mazingira katika ukanda wa Ziwa Victoria. Pichani ni waandishi wa habari waliofanya vizuri katika zoezi hilo.
Kutoka kushoto ni Bw. Deus Bugaywa kutoka gazeti la The Guardian, Katikati ni Bw. Vedastus Msungu kutoka ITV/Radio One na Kulia ni Bi. Diana Nachilonga kutoka Gazeti la Mwananchi. Hongereni

Wednesday, May 19, 2010

TIMU YA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA MWANZA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI WALIPO SHIRIKI MICHUANO YA MPIRA WA KIKAPU YA MAJIJI HUKO MOMBASA KENYA


BAADHI WACHEZAJI WA TIMU YA KIKAPU MKOA WA MWANZA "ROCK CITY" WAKIWA SAFARINI KATIKA MOJA YA VITUO KUELEKEA MOMBASA KATIKA MICHUANO YA MAJIJI YA MPIRA WA KIKAPU HUKO MOMBASA KENYA
WACHEZAJI WAKIWA WAMEVALIA NGUO ZA KUZUIA BARIDI WALIPO KUWA SAFARINI KUELEKEA MOMBASA. HII ILIWASAIDIA KUTUNZA JOTO TAYARI KUIKABILI MICHUANO.


MARA BAADA YA KUFIKA MOMBASA, HAPA WACHEZAJI WANAONEKANA WAKIELEKEA UWANJANI TAYARI KUIKABILI MICHUANO HIYO


WACHEZAJI MIPIRA NA KIKOMBE



WACHEZAJI WAKIWA KATIKA MAPUMZIKO YA VIPINDI KABLA YA MECHI KUENDELEA


TIMU YA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA MWANZA "ROCK CITY" KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WAO NDANI YA UWANJA MARA BAADA YA MICHUANO KUMALIZIKA HUKO MOMBASA NAIROBI.


WACHEZAJI NA VIONGOZI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA MICHUANO KUISHA


WACHEZAJI NA VIONGOZI KATIKA CHAKULA CHA PAMOJA KUJIPONGEZA BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA TATU KATIKA MICHUANO HIYO. HAPA NI NYUMBANI HOTEL

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MFALME WA REGGAE DUNIANI HAYATI BOB MARLEY






HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA BARABARA MBALIMBALI ZA MKOA WA MWANZA, RASTAFARIAN WAKITEMBEA NA MAGARI YALIYOKUWA YAKIPIGA MUZIKI WA REGGAE KUMKUMBUKA MFALME WA MUZIKI WA REGGAE DUNIANI HAYATI BOB MARLEY