Sunday, September 19, 2010

KASHOGI JUMA NA JUMA SHABANI VIJANA WAWILI WANAOSHINDA JALALANI KUTAFUTA RIZIKI YAO


HAPA NI JALALANI MAHALA AMBAPO VIJANA HAWA WAWILI (KASHOGI JUMA NA JUMA SHABANI) WANAPO LALA MARA BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YAO.


KASHOGI JUMA NA JUMA SHABANI WAKIWA KAZINI JALALANI



Nikiwa mkoani Mbeya niliamua kwenda kutembelea eneo la kuhifadhia taka maarufu kama dampo lilipo eneo la Uyole-Nsalaga mkoani Mbeya.
Nikiwa katika dampo hilo hilo nakutana na vijana wawili Kashogi Juma mwenye umri wa miaka 38 na mwenzie Juma shabani mwenye umri wa miaka 21. Vijana hawa wanaendesha maisha yao kutokana na kile wanachopata kutoka katika dampo hili.
Kashogi na Juma ni wakazi wa Dar es Salaam eneo la Manzese Uzuri na hapa Mbeya katika dampo hili wamekuja kufanya kazi ya kukusanya vyupa chakavu na kuvipasuapasua katika vipande vidogovidogo tayari kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa mauzo. Nilipo wauliza kwa nini kazi hii wasinge ifanya hapo hapo Dar es Salaam ama mikoa ya karibu kama Morogoro? Walinijibu kuwa Dar es Salaam na Morogoro tayari kumevamiwa na vijana kama wao ambao wanafanya kazi kama hii.
Cha kushangaza vijana hawa wanalala hapahapa Dampo kama picha inavyo onyesha. Vijana hawa wako hatarini kupata magonjwa yanayo sababishwa na uchafu kwa kuwa eneo hili lina harufu kali ya vitu vilivyo oza.
Vijana hawa huuza shilingi 80,000 kwa kila tani moja ya vyupa chakavu na shilingi 200,000 kwa kila tani moja ya Vyuma chakavu.
Vifurushi hivi husafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mauzo. Je kuna vijana wangapi wanaweza kuvumilia kufanya kazi kama hii kabla hawajafikiria kuwa wezi na majambazi ili kujipatia kipato. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?

2 comments:

  1. Yasikitisha sana lakini sasa watafanya nini kwani yote haya ni hali ya kutafuta riziki ya kila siku.

    Sio Tanzania tu bali ni kila mahali haswa Afrika kwa jumla kunao vijana wadogo (walio wacha shule/Umasikini) wanaohusika na biashara kama hiyo. Swali ni tufanye nini ili tuweze kujitoa kwa janga hili?

    ReplyDelete
  2. Anonymous said...

    Yasikitisha sana lakini sasa watafanya nini kwani yote haya ni hali ya kutafuta riziki ya kila siku.

    Sio Tanzania tu bali ni kila mahali haswa Afrika kwa jumla kunao vijana wadogo (walio wacha shule/Umasikini) wanaohusika na biashara kama hiyo. Swali ni tufanye nini ili tuweze kujitoa kwa janga hili?

    Nogrecia Nangena (Encubed )
    Nairobi-Kenya

    ReplyDelete