Tuesday, March 22, 2011
Kilele cha maadhimisho ya 23 ya wiki ya maji yafanyika kitaifa leo mkoani Mwanza , mgeni rasmi akiwa ni makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Makamu wa Rais Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal akihutubia wananchi katika maadhimisho ya 23 ya wiki ya maji yaliyofanyika kitaifa leo mkoani Mwanza, Kauli mbiu ikiwa ni MAJI KWA AJILI YA MIJI: KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI MJINI. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal amesema maadhimisho haya yanatoa fursa kwa kila mmoja wetu kutafakari wajibu wake katika dhana ya matumizi mazuri ya maji na utunzaji mazingira.
Pia Makamu wa Rais hakusita kuzitaja changamoto za utoaji wa huduma ya majisafi na majitaka kuwa ni pamoja na, kupanda kwa bei za vyuma katika soko la dunia unaosababisha upandaji wa gharama za uwekezaji katika kutoa huduma ya majisafi, uchakavu wa miundo mbinu ya kusambaza huduma ya maji,Ongezeko la watu mijini, uchafuzi wa vyanzo vya maji, uchomaji ovyo misitu na nyingine nyingi. Hata hivyo Dkt. Bilal alitoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ili kukabiliana na changamoto tulizo nazo za utoaji huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika miji yetu.
Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa baadhi ya wadau wa masuala ya maji jinsi ya kupata majisafi kupitia vyombo vya kitaalamu.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Bilal akiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark J. Mwandosya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakisiliza maelezo juu ya pampu ya maji iliyotengenezwa na watanzania kukidhi hali halisi ya mtanzania..
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa vyeti na vikombe kwa washindi wa kutunza na kuhifadhi maji kutoka makampuni mbalimbali...
Picha ya pamoja na washindi kutoka makampuni mbali mbali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment