Thursday, March 17, 2011

Sprite Basketball Bonanza in Mwanza....


Pichani (waliokaa) ni timu ya mpira wa kikapu ya BUGANDO HEAT ambao waliibuka washindi wa kwanza katika Bonanza la mpira wa kikapu lilioandaliwa na kampuni ya vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha Sprite kwa kushirikiana na chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza - MRBA. Waliosimama ni viongozi wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza wakiwa na Bwana MZIYA (Watano kutoka kulia)ambaye Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu nchini - TBF.

Pichani ni SIMON CHERU mchezaji wa Bugando Heat na pia nahodha wa timu ya mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza akipokea zawadi ya mpira baada ya kupata ushindi wa mchezaji bora 'MVP' (Most Valuable Player) katika bonanza hilo.

SIMON CHERU akiwa katika michuano ya kupiga DUNK...


Pichani ni kijana ERICK JOHN akipokea zawadi ya mpira baada ya kupata ushindi wa kuwa mpiga DUNK bora wa kwanza katika bonanza hilo...ERICKanachezea klabu ya mpira wa kikapu ya BUGANDO WORRIERS.


ERICK JOHN akiwa hewani kuelekea golini kupiga DUNK.. Wenyewe wanaita Kusafiri hewani..

Pichani anaitwa TIMOTH NGALULA mchezaji wa klabu ya mpira wa kikapu ya BUGANDO HEAT akiwa hewani tayari kwa kupiga DUNK...


Anaitwa PASCAL MAGABE kijana anayesifika kwa kuruka kupita kiasi. Pichani akijaribu kupiga DUNK kwa kutumia mipira miwili...


MOSES JACKSON akisafiri hewani kupiga DUNK... Hawa vijana ni kama wamevishwa PISTON kwenye miguu...

No comments:

Post a Comment